TPDC waanza kutafiti gesi, mafuta Mkinga

SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol nchini, TPDC limeanza utafiti wakijiolojia wa utafutaji mafuta na gesi katika vijiji vya Gombero mkoani Tanga.

Kutokana na hilo shirika hilo limeanza kutekeleza mradi wa uchongaji wa mashimo mafupi,visima vifupi kumi kwa ajili ya shughuli hiyo ya utafiti. Mradi huo unafanywa na kumilikiwa TPDC kwa asilimia 100.

Akizindua mradi huo Mgeologia, Amina Kagera alisema lengo kubwa la mradi huo ni kuwapa mafunzo wataalam vijana wa TPDC kwa kuwatumia wataalam wa ndani ya shirika waliobobea.

Alisema fursa  hiyo itawapa hamasa vijana kufanya tafiti mbalimbali nchini lengo likiwa ni uendelezaji wa utafutaji wa mafuta na gesi kwa faida ya watanzania wote.

"Mradi huu ulianza rasmi mwaka 2010 ukiwa na malengo ya kuwajengea uwezo wataalam wa sayansi ya utafutaji wa mafuta na gesi ambao hawakuwa na msingi wa taaluma ya kijiolojia kama wale wa fani ya jiofizikia na uhandisi"alisema Kagera

Kagera alisema mradi huo unahusisha wataalam wa kukusanya sampuli za jiolojia,jiokemikia na kuchambua sampuli, kufanya tafiti mbalimbali kuhusisha sampuli hizo na utengenezaji wa ramani za kijiolojia katika maeneo husika.

Alisema pia utaongeza thamani katika mabonde ya Tanzania ambapo shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi hufanyika.

"Mwaka 2012 hadi 2013 baada ya kazi za vitendo katika maeneo ya Kakindu na Mto kibindo karibu na bwawa la Nairobi,Gombero Mkoani Tanga wataalam waligundua uwepo mkubwa wa miamba tabaka aina ya Shalena,Silti Shale na makaa ya mawe" alisema Kagera

Naye Mkurugenzi wa Utafiti, Emma Msaky alisema malengo makuu ya mradi huo ni kuzidi kuyaanisha maeneo ya utafutaji wa mafuta na gesi ili kujua uwepo wa miamba ya uzalishaji wa nishati hizo.

Alizitaja gharama za uchorongaji wa mashimo hayo na visima hivyo vifupi ni takribani dola za Kimarekani 195,000 ambapo fedha zote hulipwa na TPDC kutoka kwenye mfuko wake wa fedha za miradi ya maendeleo.

Read more…

3rd TANZANIA OIL AND GAS SUPPLIERS CONFERENCE




Welcome to the 3rd TANZANIA OIL AND GAS SUPPLIERS CONFERENCE on
11th - 12th June 2015, HYATT REGENCY KILIMANJARO

Tanzania Oil and Gas Suppliers Conference (TOGSC) is a conference cum exhibition that will bring together key players from the supply chain together with stakeholders from the government and the oil and gas industry to discuss and engage on the different opportunities and challenges within the East Africa Scenario particularly Tanzania.
This conference that will incorporate suppliers within the oil and gas industry is a strategic event that has come at the right time considering the recent large and world class deposits of oil and gas in Mtwara and Lindi with potential for more to be discovered.
Within this new burgeoning oil and gas industry there is a need to bridge the gap of the supply chain between the suppliers/ service providers and the oil and gas industry Stakeholders. The conference will give suppliers especially the local Tanzanian suppliers the channels and means to harness and cater for this massive industry.
TOGSC is aimed at being the ultimate link between the Supply Chain and the stakeholders in the Oil and Gas Industry in Tanzania by empowering and building capacity. The outcomes of this conference shall assist the government in creating policies that favour the supply chain amidst them being able to be competitively being able to meet the need of the stakeholders on the Oil and Gas industry in Tanzania.
TOGSC networking events offer the opportunity to develop and strengthen your business relationships. If you’re in the Oil and Gas industry then this is a great platform for you to meet your peers – These events are attended by visitors, conference delegates and exhibitors alike.
2015 SPEAKERS
  • David L. Ross, 
    Managing director,Statera Capital Limited.
  • Mr. Richard Kasesela, 
    Chairman Mining Advisory Board,Ministry of Energy and Mineral of the United Republic of Tanzania
  • Mr. Nestory Phoye,Managing Director,Proactive Solutions (T) Ltd
  • Dr. Camillus D. N. Kassala, Lecturer & Dean of Students,Eastern Africa Statistical Training Centre
  • Mr. Peter Baziwe,Information Systems Audit and Security professional, ISACA Tanzania Chapter


Read more…