ZIARA YA NAIBU MAWAZIRI NISHATI NA MADINI, MAZINGIRA, TAMISEMI NA WABUNGE NCHINI CANADA

Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada kwa ziara ya mafunzo ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (aliyenyoosha mkono), ukiwa katika chumba cha kusimamia mitambo ya kuzalisha methano (haionekani pichani) katika kiwanda cha kuzalisha malighafi hiyo kilicho katika jimbo la Alberta nchini Canada.
Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kushoto, waliosimama), ukiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya kimataifa ya kuzalisha na kusafirisha methano ya nchini Canada mara baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika kiwanda hicho. Wengine katika picha ni Naibu Waziri, TAMISEMI, Kassim Majaliwa, (wa nne kutoka kulia, waliosimama). Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu, (wa pili kutoka kulia waliosimama) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
 

Read more…

GESI ASILIA KUOKOA BILIONI 200 KWA MWAKA


Imeelezwa kuwa Taifa litaokoa takribani Shilingi Bilioni 202 za Kitanzania kwa mwaka endapo mradi wa usambazaji wa gesi asilia katika jiji la Dar es Salaam utatekelezwa.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni mjini Dodoma katika Mkutano wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CCT), wakati Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwasilisha mada iliyohusu rasilimali za mafuta na gesi kwa manufaa ya Watanzania wote.
Akielezea mradi husika, Waziri Muhongo alisema lengo kuu ni kuweka mtandao wa mabomba ya kusambaza gesi na vituo vya kujazia gesi magari ambapo ulifanyiwa upembuzi yakinifu mwaka 2006/2007 na kuhusisha magari 8,000 na makazi yapatayo 30,000.
Profesa Muhongo alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza Julai 2015 ambapo kwa sasa zoezi la kumtafuta Mkandarasi pamoja na fedha za ujenzi takribani Dola za Marekani milioni 76 linaendelea.
 
Askofu Dkt. Valentino Mokiwa wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) baada ya Waziri huyo kuwasilisha mada katika Mkutano wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CCT).
Aidha, Waziri Muhongo alizungumzia faida iliyopatikana kitaifa kwa kutumia gesi asilia kwa kipindi cha miaka 10 kutoka mwaka 2004 na kubainisha kuwa Taifa limepata mapato kiasi cha Dola za Marekani 235.9 milioni.
Pia, alisema Taifa limeokoa kiasi cha Dola za Marekani 5.3 bilioni katika kuzalisha umeme na kiasi cha Dola za Marekani 449.7 milioni katika viwanda.
Manufaa mengine ni pamoja na Halmashauri husika hupata Kodi ya Huduma (service levy) ambayo ni asilimia 0.3 ya mapato ya mauzo ya gesi. Waziri Muhongo alitoa mfano wa mradi wa SongoSongo, ambapo Halmashauri ya Kilwa hupata takribani shilingi za Tanzania milioni 100 kila baada ya miezi mitatu.
Akizungumzia faida za bomba kuu la kusafisha na kusafirishia gesi asilia ambalo ujenzi wake unaendelea, alisema mitambo iliyopo sasa, imesababisha nchi kupoteza shilingi za Tanzania trilioni 1.6 kwa mwaka kwa kutumia mafuta kuzalisha umeme badala ya gesi asilia.
Alisema endapo bomba hili litatumika katika kiwango chake cha juu (784 mmscfd), gesi itakayosafirishwa kwa kipindi cha miaka 20 ni asilimia 12 tu ya gesi iliyogunduliwa hadi sasa.
“Nchi itaokoa Dola za Marekani bilioni moja (sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.6) kwa mwaka kutokana na mitambo iliyopo nchini inayozalisha umeme kwa kutumia mafuta kuanza kutumia gesi asilia,” alisema Waziri Muhongo.
Aidha, aliongeza kuwa bei ya uzalishaji umeme itapungua kwa uniti moja (KWh) ambapo alifafanua kuwa umeme unaofuliwa kwa dizeli na mafuta ya aina nyingine hugharimu senti za Marekani 30 hadi 45 wakati bei ya kuzalisha uniti moja hiyo hiyo ni senti za Marekani saba kwa umeme utokanao na gesi asilia.
Alizitaja faida nyingine za mradi mpya wa bomba la gesi kuwa ni pamoja na ajira katika mitambo itakayojengwa Madimba na SongoSongo kwani kila mtambo utahitaji kiasi cha wafanyakazi 60. Vilevile, alisema mradi utatoa ajira katika sekta za afya, elimu, maji usafiri pamoja na huduma nyingine za kijamii zitakazohitajika.
SOURCE;WWW.MEM.GO.TZ

Read more…